خطبة الجمعة لغات الإنجليزي الفرنساوي الألماني الأسباني الهوسا السواحيلية الروسية اليونانية

Fadhila za Kufa Shahidi na Wajibu wetu kwa Familia za Mashahidi

Fadhila za Kufa Shahidi na Wajibu wetu kwa Familia za Mashahidi

خطبة الجمعة القادمة لوزراة الأوقاف المصرية والخطبة المسموعة باللغة السواحيلية : فضل الشهادة ، وواجبنا نحو أسر الشهداء ، 24 يناير 2020 م ، 29 جمادي الأولي 1441 هـ .

 

video

 

 

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote, anaesema katika Qurani tukufu:

{وَلاَ تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاء عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ * فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللّهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُواْ بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلاَّ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ* يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللّهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللّهَ لاَ يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ}

Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumuini.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata mpaka siku ya Mwisho.

Na baada ya Utangulizi huu:

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuumba mwanadamu kwa ajili ya kuijenga Ardhi na kuitengeneza, na Mwenyezi Mungu Mtukufu na Msema kweli akamuhifadhia Mwanadamu yale yanayomsaidia ujenzi huo, na akaizungushia nafsi ya mwanadamu ambayo ndiyo niia ya kumkalifisha, akaizungushia Uzio wa Ulinzi Uzio ambao umemfanya adui yoyote dhidi yake au uharibifu wowote Ardhini ukawa ni sawa na uadui kwa Watu wote.na aina yoyote ya lindo la nafsi au utengenezaji wowote Ardhini ni Ulinzi kwa Watu wote. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا}.

ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.

Na lengo la Ujenzi wa Dunia na Uhuishaji wake ni katika Malengo yenye thamani ya juu mno ambalo hakipatikani isipokuwa kwa kujitoa muhanga kwa kiasi kikubwa, kwa wale wenye nia njema kwa ajili ya Dini na Nchi yao, wale ambao walitambua kitambo thamani ya Dini na Nchi yao na Maisha ya Usalama na Amani yaliyo tulivu. Wakajitolea kwa mali na kwa nafsi zao ili kulifikia lengo hili na wakaingia kwenye biashara yenye faida na Mola wao Mtukufu, nayo ni biashara isiyo na hasara, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنْفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ}

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu – wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur’ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Na Malipo yao yakawa sawa na matendo yao; ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawafanikishia Malipo yaliyo bora kuliko waliyoyatarajia kuwawekea wengine, kwa nia yao njema, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawalipa Maisha ya Milele yenye Usalama, Amani na Utulivu wa Kudumu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلاَ تَقُولُواْ لِمَنْ يُقْتَلُ فِي سَبيلِ اللّهِ أَمْوَاتٌ بَلْ أَحْيَاء وَلَكِن لاَّ تَشْعُرُونَ}.

Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui.

Na kufa Shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni nafasi miongoni mwa nafasi za juu, na ni lengo miongoni mwa malengo ambayo hayapatikani isipokuwa kwa wateule aliyowachagua Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Waja wake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَيَتَّخِذَ مِنْكُمْ شُهَدَاءَ}

…na awateuwe miongoni mwenu mashahidi.

Hakika hili ni tuzo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuelekea kwa vipenzi vyake katika viumbe wake baada ya Mitume, na Wakweli, kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقًا}

Na wenye kumt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!

Vilevile Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaokoa kutokana na fitina Kaburini na Ukele wa Siku ya Malipo, na Mtu mmoja alimuuliza Mtume S.A.W, akasema: Ewe Mtume Wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni ipi hali ya Waumini wanofitinishwa katika Makaburi yao isipokuwa Shahidi? Akasema Mtume S.A.W: mwangaza wa panga juu ya vichwa vyaounatosha kuwa ni fitina.

Na Mtume S.A.W, alipomuuliza Jiburilu A.S, kuhusu Aya hii:

كما أن الله سبحانه ينجيهم من فتنة القبر، ومن الصعق يوم القيامة ، فقد قال رجل : يَا رَسُولَ اللهِ ، مَا بَالُ الْمُؤْمِنِينَ يُفْتَنُونَ فِي قُبُورِهِمْ إِلَّا الشَّهِيد؟ قال (صلى الله عليه وسلم) : (كَفَى بِبَارِقَةِ السُّيُوفِ عَلَى رَأْسِهِ فِتْنَةً) ، ولما سأل النبي (صلى الله عليه وسلم) جبريل (عليه السلام) عن هذه الآية :

{وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَمَنْ فِي الأَرْضِ إِلا مَنْ شَاءَ اللَّهُ}

Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipo kuwa aliye mtaka Mwenyezi Mungu.

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. NaNa ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata mpaka siku ya Mwisho.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika katika Wajibu wetu, ni: Ni kuwaandalia Maisha Mazuri yenye usalama na utulivu, kwani wazazi wao wamekufa Mashahidi kwa ajili ya kutuandalia sisi Maisha haya tuliyonayo, na Mtume S.A.W, amemuhakikishia mtu yoyote anayebeba jukumu la kuzilea familia za Mashahidi na watoto wao, amewahakikishia thawabu na Malipo mazuri ambapo anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakayemwandalia Mpiganaji mahitaji yake ya kivita basi na yeye atakuwa amepigana vita, na atakayeiacha vita kwa ajili ya heri ya familia yake basi atazigatiwa na yeye ni mpiganaji na atalipwa malipo ya mpiganaji vita. Kutoka kwa Zaid bin Aslam, kutoka kwa Baba yake, anasema: Nilitoka na Omar R.A, tukaenda gulioni, na  Mwanamke Mmoja mdogo kiumri, akamfuata Omar na akasema: Ewe Amiri wa Waumini, mume wangu ameangamia na ameacha watoto wadogo, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, watoto hao hawajui kupika wala kujitafutia riziki na wala hawana shamba na nikachelea wasije wakafa kwa njaa kutokana na kutokuwa na chakula na mimi ni Bintiye Khufaafi bin Iimaail Ghiffaariy, na Baba yangu amekufa Shahidi katika vita vya Hudaibiyah alipokuwa na Mtume S.A.W. Omar R.A, akasimama nae kwa muda, na hakukaa sana akasema: Ninaikaribisha nasaha hii ya karibu, kisha akamwelekea ngamia wake aliyekuwa amefungwa kamba nyumbani, akambebesha vikapu viwili alivyovipata chakula, na akabeba baina ya vikapu hivyo viwili, vitu vya kutumia na nguo kisha akampa na kamba ya mnyama huyo na akamwambia: mwomgoze hadi nyumbani na hataisha isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa amekujaalieni heri nyingi. Yule mtu aliyekuwa na Amiri wa Waumini akasema: Ewe Amiri wa Waumini huoni kama umemzidishia huyo mwanamke? Omar R.A, akasema: Maneno gani hayo unayoyasema? Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakika mimi ninamwona baba yake huyu na nduguye wameizingira ngome kwa muda kisha wakaivamia kisha Sisi tukawa tunagombea walichokivuna ndani ya ngome hiyo.

وَاللهِ إِنِّي لأَرَى أَبَا هَذِهِ وَأَخَاهَا قَدْ حَاصَرَا حِصْنًا زَمَانًا فَافْتَتَحَاهُ ثُمَّ أَصْبَحْنَا نَسْتَفِيءُ سُهْمَانَهُمَا فِيهِ).

Katika Tukio hili, tunamwona Omar R.A, Amiri wa Waumini akitubainishia yanayotulazimu kwa Mashahidi wetu kama vile kuyatambua Mazuri yao na mema waliyoyafanya, na anatubainishia vilevile Wajibu wetu kwa familia zao, jambo ambalo linaweza kutafsiriwa katika zama zetu Kama mchango muhimu wa kila mtu na hata taasisi wa kuwalea watoto wao, kwa maana kamili ya kuwalea, kwa kuwaridhia wao, na kwa kutambua mazuri yao. Na miongoni mwa hayo ni: Kuwaandaa vizuri watoto wao, na kuwaweka wenye wale Wenye Uwezo katika nafasi zao wanazozistahiki. Na sisi tuna kigezo kizuri ambacho ni Mtume S.A.W; kwani yeye alikuwa anatoa ahadi kwa familia za Mashahidi, kuzilea na kuzilinda, na alikuwa anawaandaa watoto wao kwa maandalizi yalio bora zaidi, na mfano wake ni jinsi Mtume S.A.W, alivyokuwa na Bwana wetu Usama bin Zaidi, Kwani baba yake ambaye ni Zaid bin Haarith R.A, alikufa Shahidi katika vita vya Mu-utah na Mtume S.A.W, akaahidi kumlea Usama na kumsomesha, mpaka akaja kuwa kiongozi wa kijeshi mwenye Umri mdogo katika Historia yote! Alikuwa bado hajafikisha miaka ishirini, ambapo Mtume S.A.W, alimpa uongozi wa Jeshi ambalo lilikuwa na Maswahaba wakubwa, na Mtume S.A.W, alisema: Mkiupinga uongozi wake wa Jeshi, basi mtakuwa mmeupinga uongozi wa baba yake, aliyeongoza hapo kabla yake ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika yeye alikuwa Kiongozi, ingawa alikuwa kipenzi changu, na hakika huyu ni miongoni mwa vipenzi vyangu baada ya Baba yake. Na tunazipa habari njema familia zote za Mashahidi na watoto wao pia, kuwa wako katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ulezi wake anajaalia kutengemaa kwa wazazi iwe faida kwa watoto wao Duniani na Akhera. Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwawekea Vijana wawili mayatima, aliwawekea Waja wake wawili ambao ni Mtume Musa A.S, na Khidhri A.S, ili wawahifadhie vijana hao mali na hazina yao, kama heshima kwa Wazazi wao Wema ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنزٌ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنزَهُمَا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي}

Na ama ukuta, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako khazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu.

Ama kwa upande wa Akhera Mola wao Mlezi atawapelekea wazazi wao kama ni njia ya kuwaadhimisha hata kama matendo yao yatakuwa machache. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُمْ بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُمْ مِنْ عَمَلِهِمْ مِنْ شَيْءٍ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ}.

Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima apate alicho kichuma.

Na Sisi tunapaswa kujua kwa uyakinifu ya kwamba kujitokea kwetu na kufa Shahidi taji  kwenye kichwa cha taifa letu na katika paji la kila mwananchi mwenye nia njema na Nchi yake. Na kwamba utekelezaji wa kazi hizi za kujitoa mhanga kumhitaji kila mmoja wetu awe bega kwa bega katika nyanja zake, na atumie nguvu zake kiasi awezacho katika kuitumikia Nchi tukufu, na tusimame sote bega kwa bega kwa moyo mmoja nyuma ya jeshi letu la Ulinzi na na la Usalama pamoja na nyuma ya taasisi zote za nchi. Huku tukiwa na uhakika kwamba taasisi zetu zote za taifa ziko imara kwa ajili ya Usalama wa Jamii na kwamba Sisi sote tunapaswa kupambana na walinganiaji wa fitina na machafuko, miongoni mwa makundi yenye Siasa kali na ya kigaidi ambayo hayaamini Taifa wala Utaifa, bali wanatanguliza maslahi yao binafsi dhidi ya masilahi ya nchi, makundi Kama haya ni hatari inayoinyemelea Dini na Nchi na kupambana nao na kuzifyeka fikra zao za kigaidi ni wajibu wa Kidini, kinchi na kibinadamu.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape Mashahidi wetu rehema pana zaidi na alinde na Shari Nchi yetu Pendwa na iliyo Tukufu, Majeshi yetu ya Usalama na ya Ulinzi wa Nchi, na wananchi wote.

 

_____________________________

للإطلاع علي قسم خطبة الجمعة

 

تابعنا علي الفيس بوك

 

الخطبة المسموعة علي اليوتيوب

 

للإطلاع علي قسم خطبة الجمعة باللغات

 

للإطلاع ومتابعة قسم خطبة الأسبوع

 

للمزيد عن أخبار الأوقاف

 

للمزيد عن أسئلة امتحانات وزارة الأوقاف

 

للمزيد عن مسابقات الأوقاف

اظهر المزيد

كتب: د.أحمد رمضان

الدكتور أحمد رمضان حاصل علي الماجستير من جامعة الأزهر بتقدير ممتاز سنة 2005م ، وحاصل علي الدكتوراه بتقدير مع مرتبة الشرف الأولي من جامعة الأزهر الشريف سنة 2017م. مؤسس جريدة صوت الدعاة ورئيس التحرير وكاتب الأخبار والمقالات المهمة بالجريدة، ويعمل بالجريدة منذ 2013 إلي اليوم. حاصل علي دورة التميز الصحفي، وقام بتدريب عدد من الصحفيين بالجريدة. للتواصل مع رئيس التحرير على الإيميل التالي: [email protected] رئيس التحريـر: د. أحمد رمضان (Editor-in-Chief: Dr. Ahmed Ramadan) للمزيد عن الدكتور أحمد رمضان رئيس التحرير أضغط في القائمة علي رئيس التحرير

اترك تعليقاً

لن يتم نشر عنوان بريدك الإلكتروني. الحقول الإلزامية مشار إليها بـ *

هذا الموقع يستخدم Akismet للحدّ من التعليقات المزعجة والغير مرغوبة. تعرّف على كيفية معالجة بيانات تعليقك.

زر الذهاب إلى الأعلى
Translate »