Jinsi ya kuitumia Misimu ya Ibada na Kheri
Jinsi ya kuitumia Misimu ya Ibada na Kheri
خطبة الجمعة لوزراة الأوقاف مسموعة باللغة السواحيلية : اغتنام مواسم الطاعات والخيرات خطبة الجمعة القادمة غرة ذي الحجة ، 2 أغسطس 2019 م ، غرة ذي الحجة 1440 هـ
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, anayesema katika Kitabu chake Kitukufu:
{وَسَارِعُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ * الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ}
Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu, Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema;
Na ninashuhudia kuwa hapana mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu msalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata mpaka siku ya Malipo.
Na baada ya Utangulizi huu:
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametenga katika masiku ya mwaka mzima, misimu ya kufanya ibada ambayo ndani yake malipo huongezeka kwa wingi mkubwa, na huzidi kheri ndani ya misimu hiyo, na daraja hupandishwa kwa ajili ya kuhimiza watu wadumu katika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu lakini pia na kuipokea misimu hiyo vyema.
Na mwenye akili ndiye anayeweza kuitumia misimu hiyo vilivyo na akaisafisha nia yake na akatenda mema ndani ya misimu hiyo kwa uzuri wa kutenda na akamwelekea Mola wake Mtukufu kwa kuongeza mambo ya kheri na akapata tunu na rehma zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo anasema Mtume wetu Muhammad S.A.W: Hakika Mola wetu Mtukufu ana yeye katika masiku ya mwaka wenu masiku ya tunu, basi yapateni masiku hayo, huwenda mmoja wenu akaipata moja kati ya hizo tunu na baada ya tunu hiyo hawi mwovu milele.
Na katika mambo yasiyokuwa na shaka ni kwamba sisi tunaishi katika masiku haya msimu miongoni mwa misimu mitukufu ya kulipwa kwa wingi, na yenye uzito mkubwa, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia thawabu za mema ndani ya masiku haya kuwa nyingi mno, na malipo makubwa ya kazi ndani ya masiku haya ni tofauti na masiku mengine, kwani haya masiku ni matukufu, na ni nyakati zilizotukuzwa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amezinyanyua daraja, na Mtume S.A.W amefafanua nafasi ya masiku haya, na kwa ajili hiyo: Mwenyezi Mungu Mtukufu ameapa katika Qurani tukufu ambapo anasema:
{وَالْفَجْرِ* وَلَيَالٍ عَشْرٍ * والشفع والوتر}
(Naapa kwa alfajiri, Na kwa masiku kumi, Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja.)
Na rai wanayoifuata wanazuoni wote ni kwamba Masiku haya kumi ni ya mwanzo wa mwezi wa Dhulhijja, na Mwenyezi Mungu Mtukufu haapi isipokuwa kwa kitu kitukufu, na kiapo kilichopo hapa ni kwa lengo la kuyatukuza masiku hayo na kuonesha nafasi yake, na kuwazindua waja kuyahusu masiku haya, na kuweka wazi fadhila zake, na kuwaongoza katika umuhimu wake.
Na miongoni mwa fadhila zake: ni kuwa masiku haya yanajulikana kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu anaposema:
{وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَعْلُومَاتٍ عَلَى مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ}
(… na walitaja jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama yao alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri). Kwa hiyo masiku haya ndani yake humkusanyikia Mwislamu aina mbali mbali za ibada, ambapo yeye huwa na nafasi ya kutekeleza ibada hizo kama vile swala, sadaka, swaumu, na Hija, na ibada hizi haziji hivyo katika masiku mengine kinyume na haya.
Na katika fadhila za masiku haya ni kwamba:
Ni masiku ayapendayo mno Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kazi yoyote nzuri ndani ya masiku haya inapendwa mno na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko katika masiku mengine. Huu ni msimu wa mapato, na ni njia ya uokovu na ni uwanja wa kushindana katika mazuri ambapo anasema Mtume S.A.W: Hakuna masiku ambayo kazi njema inapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu kama katika masiku haya. Kwa maana ya masiku kumi. Maswahaba wakasema:
Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake na hakurejea kutokana na hicho kilichomtoa. Kwa hivyo kila Mwislamu anapaswa kuyatumia masiku haya yenye fadhila kubwa mno, na malipo makubwa sana kwa kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila aina za ibada na kumtii yeye.
Na miongoni mwa matendo yaliyo bora na ya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya masiku haya, ni kuhiji Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu mtukufu kwa mwenye kuweza kufanya hivyo.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَعْلُومَاتٌ فَمَنْ فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ}
Hijai ni miezi maalumu. Na anayekusudia kufanya Hijai katika miezi hiyo basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala sibishane katika Hija.
Na Hija ni nguzo ya tano ya Uislamu ambayo kwayo jambo hili hutimia, na dhambi husameheka, na Mja huandikiwa mazazi mapya ambapo Mtume S.A.W anasema: Mtu yoyote atakayehiji na akawa hakufoka maneno machafu na wala hajafanya mabaya yoyote, basi atarejea na kuwa kama siku aliyozaliwa na mama yake.
Na Hija ni mnasaba Mkubwa kwa ajili ya kujifunza fadhila nyingi na Maadili mema, ambapo mwislamu analeleka ndani yake katika kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujilinda na misukumo na matamanio ya nafsi yake pamoja na kujipamba na tabia njema na mazuri yake kwa kuwapendelea watu na sio kujipendelea, na kutosheka na kutotamani vya watu, sio kuomba omba wala kufanya israfu.
Mwislamu pia anajifunza ndani ya masiku haya uhakika wa maneno na vitendo vyake, pamoja na kukufuata sheria na kujidhibiti. Kwa hivyo, Mtu anayehiji ni wajibu kwake ndani ya masiku ya Hija kutekeleza kivitendo yale yanayolinganiwa na Uislamu miongoni mwa Maadili mema, na Tabia Njema; ili atoke katika chuo cha Hijai akiwa amenufaika na madhumuni yake ya kimaadili na kimwenendo.
Sisi tunathibitisha kwamba Ibada ya Hijai ni Ujumbe wa Amani kwa Ulimwengu wote. Hijai ni Amani kwa ujumla, na Usalama kwa Ujumla. Kwani Mwenyekuhiji hagombani na yoyote, wala hamwindi mnyama wala hamuudhi au hata kumuua.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنْتُمْ حُرُمٌ}
Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija.
Na wala haiishii katika kuwa na amani na Watu na Wanyama tu bali hali hii inaelekea na kutanda pia kwa mimea. Mwenye kuhiji anaamrishwa awe na amani hata kwa mimea ambapo anasema Mtume S.A.W: Hakika Nchi hii Mwenyezi Mungu ameharamisha ndani yake kutokatwa hata mwiba, na wala mnyama yoyote asibughudhiwe, na mnyama aliyepotea asiokotwe isipokuwa na mtu anayemjua.
Na hapana shaka kwamba katika hayo yote kuna mafunzo na maandalizi kwa mwislamu ili Watu, Miti, na hata Mawe visalimike na maudhi yake baada ya kurejea kwake kutoka katika utekelezaji wa Ibada ya Hijai. Na Mtume S.A.W ametuambia kuwa Mwislamu wa kweli ni yule ambaye Watu watasalimika na Ulimi wake na Mkono wake. Ambapo anasema Mtume S.A.W katika Hotuba yake ya Kuaga: Je nikujulisheni kuhusu Muumini? Ni yule ambaye watu wamemwamini kwa mali na nafsi zao, na Mwislamu:
ni yule ambaye Watu wamesalimika na Ulimi pamoja na Mkono wake. Na Mpiganaji Jihadi: ni yule ambaye anapambana na Nafsi yake katika Kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Muhaajir (Mhamaji): ni yule aliyehama makosa na Madhambi.
Na katika vitendo vyenye fadhila nyingi ambavyo inapendeza kwa Mja kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu kwa vitendo hivyo katika masiku haya, ni: Swaumu. Swaumu ni katika vitendo bora vya kumtii Mwenyezi Mungu na ni njia bora ya kujikurubisha kwake. Na Mwenyezi Mungu ameiongeza ibada hii kwake yeye kutokana na uzito wa hadhi yake na utukufu wa hceo chake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi Qudsiy: Kila kitendo cha Mwanadamu ni chake yeye isipokuwa Swaumu ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa.
Na Mtume S.A.W anasema:
Mja yoyote atakayefunga siku moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atauepusha Uso wake na Moto kwa kiasi cha miaka sabini. Na kwa hivyo inapendeza kwa Mwislamu afunge siku Tisa za Mwezi wa DhulHijai kiasi awezacho. Na kuzifunga siku hizo ni katika vitendo avipendavyo mno Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hasa Siku ya Arafa kwa siyehiji. Mtume S.A.W ametenga swaumu ya siku hii ya Arafa miongoni mwa masiku kumi ambapo anasema S.A.W:
Swaumu ya Siku ya Arafa humwa ninamtegemea Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu ya Mwaka mzima ulio kabla yake na mwaka mzima ujao baada yake. Na siku ya Arafa ni katika masiku ya Mwenyezi Mungu Mtukufu yanayoshuhudiwa kujitokeza kwa Utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake, kwa Rehma, Kusamehe makosa yao na kuwaacha huru na Moto. Ni siku ambayo ndani yake hujibiwa Maombi ya waja na makosa madogo madogo husamehewa, na Mwenyezi Mungu hujigamba kwa viumbe vya Ardhini na Mbinguni. Anasema Mtume S.A.W:
Hakuna siku ambayo Mwenyezi Mungu kwa wingi humuepusha ndani yake mja wake na Moto kuliko siku ya Arafa, na hakika yeye Mwenyezi Mungu huwajongelea waja wake kisha kisha akajigamba kwa malaika, nayo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliikamilisha Dini yake ndani ya siku hii, na kuikamilisha neema yake. Kutoka kwa Omar bin Khatwaab R.A: kwamba kuna mtu mmoja katika Mayahudi alisema: Ewe Amiri wa Waumini, kuna aya moja imo ndani ya Kitabu chenu mnaisoma, kama tungekuwa tumeteremshiwa sisi Mayahudi basi siku hiyo ya kuteremshwa kwake tungeifanya ikawa Sikukuu. Akasema: Ni aya ipi hiyo? Akasema yule Myahudi:
{الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا}
Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.
Akasema omar R.A: Tumejua hivyo leo, na sehemu ilipoteremshiwa kwa Mtume S.A.W, hali ya kuwa amesimama Arafa, siku ya Ijumaa.
Inapendeza pia kwa Mwislamu kukithirisha utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika masiku haya, kwani kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ni uhai wa Nyoyo, na kwa utajo wa Mwenyezi Mungu hupatikana Utulivu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُمْ بِذِكْرِ اللَّهِ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ}
Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!
Na Mtume wetu S.A.W anasema: Hakuna masiku yaliyo bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu wala amali inayompendeza zaidi yeye ndani ya masiku hayo kuliko masiku haya kumi.
Zidisheni ndani yake utajo wa Mwenyezi Mungu wa tahliili (Laa ilaaha illa Llaahu), na utajo wa Takbiiraa (Allaahu Akbar), na utajo wa Tahmiid (alhamdulillah). Na Bwana wetu Omar R.A alikuwa akitoa Takbiira katika eneo la mbele la msikiti na watu wakawa wanamsikia na wao wanatoa Takbiira kwa kusema: Allaahu akbar. Na watu wa Masokoni nao wanatoa Takbiira mpaka eneo lote la Mina linatikisika kwa Takbiira.
Na Omar R.A alikuwa anatoa Takbiira katika anapokuwa Mina ndani ya masiku hayo kbla ya kila swala na hata akiwa kitandani kwake, anapoketi, au anapotembea, na kwa ajili hiyo inapendeza kwa Mwislamu atoe Takbiira kwa sauti katika masiku haya kwa ajili ya kuutangaza na kuudhihirisha utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mtume wetu S.A.W: Je nikujulisheni kilicho bora katika matendo yenu, na kilicho na daraja za juu zaidi, na kilicho takasika mbele ya Mola wenu Mfalme wa Ulimwengu, na ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha, na ni bora zaidi kwenu kuliko kukutana na adui zenu na mkazikata shingo zao? Wakasema: ndio. Akasema: Ni kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kutoka kwa Muaadh bin Jabal R.A, Hakuna kazi bora ya mwanadamu inayomwokoa zaidi na adhabu ya Mwenyezi Mungu kuliko kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ninayasema maneno yangu haya, na ninamwomba Msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili yangu na kwa ajili yenu
* * *
Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ninashuhudia kuwa hapana mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu msalie, mrehemu na umbariki yeye Mtume wetu, na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.
Ndugu zangu Waislamu. Hakika miongoni mwa matendo yanayomkurubisha zaidi Mja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika masiku haya: Ni kichinjo. Kichinjo ni moja ya Alama za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nayo ni alama ya Dini ya Ibrahim A.S. Na ni dalili ya Sunna ya Muhammad S.A.W.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَـائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوب}
Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.
Mtume S.A.W alipoulizwa: Nini hivi vichinjo? Akasema: Ni Sunna ya Baba yenu Ibrahim. Na anasema Mtume S.A.W: Hakuna siku ya mwanadamu katika siku ya kuchinja inampendeza zaidi Mwenyezi Mungu kuliko kuchinja. Na hakika mambo yalivyo, kichinjo kitakuja siku ya Kiama kikiwa na mapembe yake, na manyoya yake na kwato zake, na kwamba damu yake itadondokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika sehemu kabla ya kudondoka kutoka ardhini, basi zipambeni nafsi zenu kwa vichinjo.
Kuchinja ni sura miongoni mwa sura za kuleana kijamii ambazo huleta mapenzi, na kuhurumiana, na kufungamana baina ya wanajamii wote. Na Mtume S.A.W alipoona watu wana utapia mlo, akawaambia: yoyote atakayechinja miongoni mwenu basi asipambazukiwe hadi siku ya tatu akiwa amebakiza kitu katika kichinjo chake
Na uliwadia mwaka mwingine wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, tufanye kama tulivyofanya mwaka uliopita? Akasema: Kuleni na wekeni akiba, kwani mwaka jana watu walikuwa na njaa sana na nikakutakeni msaidie ndani ya Mwaka huo.
Maisha yanapokuwa mazuri na Watu wana uwezo basi hutumika kauli ya Mtume S.A.W isemayo: Kuleni, toeni sadaka na wekeni akiba. Na pindi Watu wanapokuwa na haja zaidi au wakiwa na utapia mlo basi itumieni kauli ya Mtume S.A.W isemayo: Yoyote miongoni mwenu atakayechinja basi asipambazukiwe baada ya siku ya tatu hali ya kuwa nyumbani kwake kuna kitu chochote katika kichinjo.
Kwa kujua kuwa kama ambavyo kichinjo kunapatikana kwa kuchinja, kinatikana pia kwa kununua kununua kwa wingi, na hakuna shaka yoyote kuwa kufanya hivyo ni katika kuleta manufaa ya kuchinja na hasa kwa yule asiyekuwa na chombo cha ugavi kwa njia nzuri zaidi, jambo ambalo hukifanya kichinjo kifika kwa njia ya kununua kwa wingi hadi kuwafikia walengwa wenyekustahiki,
jambo ambalo huongeza manufaa ya Kichinjo na thawabu zake kwa wakati huo huo, na pia huchangia katika kuifikisha kheri kwa wenyekustahiki, kwa hadhi na heshima yao, na nia uzuri ulioje wa mwenye kuweza tena mwenye mali kukutanishwa na mambo mawili ya kuchinja kichinjo kwa ajili ya kupanua zaidi kwa Jamaa zake na nduguze, pamoja na kununua kwa wingi kama ni upanuzi kwa mafukara wote katika maeneo yenye kuhitaji zaidi
Mwislamu anapaswa kuzidisha kwa wingi aina mbali mbali za kheri ambazo zinaweza kuwanufaisha watu wote. Azidishe kutoa sadaka ili aingize faraja na furaha katika nyoyo za mafukara na wenyekuhitaji.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu, ametuasa sisi kuifanya ibada ya kutoa, akasema:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَنفِقُواْ مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لاَّ بَيْعٌ فِيهِ وَلاَ خُلَّةٌ وَلاَ شَفَاعَةٌ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ}
Enyi mlio amini! Toeni katika tulivyo kupeni kabla haijafika Siku ambayo hapatakuwapo biashara, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio madhaalimu.
Na katika Hadithi ya Mtume S.A.W: Haipungui mali ya mja kwa kutoa sadaka.
Tuna hitaji kwa kiasi kikubwa mno Kuleana na Kuhurumiana, na kila mmoja kumuhisi mwingine, kwa kutekeleza kauli ya Mtume wetu S.A.W aliposema: Mwislamu ndugu yake ni Mwislamu; hamdhulumu, wala hamdhuru. Na yoyote atakayemsaidia ndugu yake basi Mwenyezi Mungu atamsaidia yeye. Na yoyote atakaemwondoshea jambo zito ndugu yake Mwislamu, katika mambo mazito basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamwondoshea yeye jambo zito siku ya Kiama. Na yoyote atakayemsitiri mwislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu naye atamsitiri Siku ya Kiama.
Na anasema Mtume S.A.W: Kila Mwislamu ana sadaka. Maswahaba wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kama mtu hakupata cha kukitoa sadaka je? Akasema: basi afanye kazi kwa mikono yake, na ajinufaishe yeye na kisha atoe sadaka. Wakasema Maswahaba: Na ikiwa hakupata je? Akasema: atamsaidia mwenye shida aliyekwama. Wakasema: na kama hakupata je? Akasema: basi atende mema na ajizuie na shari, kwani hayo kwake ni sadaka.
Ewe Mola wetu tunakuomba utusaidie sisi tuwe ni wenye kukutaja, na kukushukuru na kukuabudu vyema
_____________________________
للإطلاع علي قسم خطبة الجمعة باللغات
للإطلاع ومتابعة قسم خطبة الأسبوع
للمزيد عن أسئلة امتحانات وزارة الأوقاف